NJIA 10 ZA KUJIOKOA NA KIMBUNGA

Reads: 160  | Likes: 0  | Shelves: 0  | Comments: 0

  • Facebook
  • Twitter
  • Reddit
  • Pinterest
  • Invite

Status: Finished  |  Genre: Non-Fiction  |  House: Booksie Classic

Kimbunga ni dhoruba kali inayoanza juu ya bahari katika maeneo ya tropiki yenye upepo wenye kasi. Sawa na malaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga Jobo ambacho kasi yake sawa na taarifa ya TMA imepungua kutoka kilomita 12 kwa saa ya awali hadi kilomita 6 kwa saa, sawa na taarifa ya tarehe 23 April 2021. Kutokana na hali hiyo Kimbunga Jobo kinatarajia kuingia nchi kavu tarehe 25/04/2021 Jumapili majira ya mchana na kuikumba mikoa ya pwani (Lindi, Tanga, Dar es Salaam na Mtwara (maeneo mengine ni Mafia Pemba na Unguja)).

NJIA 10 ZA KUJIOKOA NA KIMBUNGA

Na Mbega R. Ngata

Email: ngatambega41@gmail.com

 

Kimbunga ni dhoruba kali inayoanza juu ya bahari katika maeneo ya tropiki yenye upepo wenye kasi. Sawa na Malaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga Jobo ambacho kasi yake sawa na taarifa ya TMA imepungua kutoka kilomita 12 kwa saa za awali hadi kilomita 6 kwa saa, sawa na taarifa ya tarehe 23 April 2021. Kutokana na hali hiyo Kimbunga Jobo kinatarajia kuingia nchi kavu tarehe 25/04/2021 Jumapili majira ya mchana na kuikumba mikoa ya pwani (Lindi, Tanga, Dar es Salaam na Mtwara (maeneo mengine ni Mafia Pemba na Unguja)).

Nimeona ni jambo zuri na vyema kukumbushana njia 10 za kujiokoa wakati wa Kimbunga kama kitaleta madhara ili kuokoa maisha na kupunguza madhara hasa kwenye maeneo ambayo Kimbunga Jobo kinapita. Sawa na hali zetu na mazingira ya nyumba zetu ni muhimu kuzingatia njia ninazo taka kuzieleza. Zifuatayo ni njia za kuzingatia endapo Kimbunga Jobo kitafanikiwa kufika kwa kasi kwenye maeneo yetu.

1. HAKIKISHA UNAKUA NA TAARIFA KAMILI KUTOKA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA (TMA) WAKATI WOTE.

Kuwa na taarifa sahihi ni njia moja wapo wa kujilinda wewe pamoja na familia yako kwa maana utaweza kufupisha mizunguko yako na kusitisha mizunguko yote ya familia yako na kuwapo taarifa ndugu na jamaa zako. Kwa taarifa Zaidi unaweza kuingia tovuti ya mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (https://www.meteo.go.tz/) au kufuatilia matangazo yao yanayo yatoa mara kwa mara.

 

ZIMA SWICHI ZOTE ZA UMEME, GESI NA MAJI

Kimbunga huwa na kasi kubwa hivyo huweza kusababisha nyanya kugusana na kusababisha mlipuko wa umeme hatimaye kusababisha moto kutokea. Vile vile mitungi ya gesi huweza kuanguka na kusababisha gesi kuvuja, hii itapelekea kutokea mlipuko wa moto kwa sababu kutakua na msuguano wa bati au milango au madirisha kwa upepo mkali ambayo husababisha cheche za moto na kuweza kudaka kwenye gesi. Pia maji huweza kuzibuka kwa nguvu. kama hujafunga koki hupelekea kumwagika au kujaza choo au nyumba nzima kwa wale wenye mabomba ya ndani. Uzimaji wa swichi za umeme, gesi na hakikisha unafanya mtu mzima na si kumwachia mtoto mdogo.

 

3. WEKA VIZUIZI KWENYE MILANGO NA MADIRISHA

Hakikisha milango na madirisha yako unayashikiza vizuri kwa kuyaongezea uwezo wa kujishikiza ili kuhimili upepo mkali. Unashauriwa usikae karibu ya mlango baada ya kufanya kuweka vishikizi. Unaweza tumia kitu kizito kuweka nyuma ya mlango au mbao kubwa. Unaweza kufanya kwenye madirisha na sehemu za wazi pia kwa sababu kama upepo ukiweza kuingia ndani kwa kasi unaweza kufumua nyumba au kuingiza maji Zaidi ndani ya nyumba.

N.B

Usikae kwenye mlango wala madirisha kwani si salama wakati upepo mkali.

 

 

4. TAARISHA DAWA MUHUMU KWA HUDUMA YA KWANZA

Kuwa na dawa za huduma ya kwanza ni muhimu sana wakati wa dhoruba kwa maana inaweza kutokea tatizo lolote na kupelekea mtu kupata jeraha, kupata mshituko au ugonjwa wowote wa ghafla kipindi cha kimbunga au baada ya kimbunga kwa sababu uwezi fahamu kama athari ya kimbunga itasababisha huduma kuchelewa kupata/kushindwa kufika hospitalini au kwenye huduma ya afya au duka la dawa muhimu.

 

 

5. ENDELEA KUSIKILIZA MWENENDO WA KIMBUKA KWA REDIO AU MTANDAO

Usijifungie ndani bila kuwa na chanzo cha taarifa kwa maana kama kimbunga kimeongezeka kunaweza kuwa na wazo la kuwaondoa watu wa sehemu fulani na kuwapeleka sehemu nyingine basi unaweza kujua na kufahamu mwenendo mbali mbali na uelekeo wa Kimbunga. Hivyo kusikiliza habari ya mwenendo wa kimbunga ni muhimu sana. Hakikisha una chaji au mabetri ya redio ya kutosha kuepuka kukosa taarifa muhimu.

 

6. USIKATIZE KWENYE DIMBWI LOLOTE LA MAJI

Watu wengi hupenda kupita katikati ya maji yaliyo twama. Uwenda kwenye dimbwi hilo kuna shimo, bati, mbao za misumali au mmomonyoko wowote ulitokea kwa sababu ya kimbunga hivyo utaatarisha usalama wako. Ni vyema kupita baada ya kujiridhisha au kupita sehemu nyingine kwa usalama zaidi

 

7. MUDA WOTE MZAZI HAKIKISHA UPO KARIBU NA WATOTO WAKO

Mzazi usiwaache watoto wakae chumba kingine kwa sababu mara nyingi watoto hupenda kuchungulia nje kuangalia nini kinaendelea hvyo huweza kufungua madirisha au kuwasha umeme hata gesi jikoni na kusababisha hatari. Hakikisha upo na watoto wako muda wote hasa wale wadogo.

 

8. OMBA HIFADHI KWENYE NYUMBA IMARA

Kama nyumba yako unaona sio imara basi unashauriwa kuomba hifadhi kwa jirani mwenye nyumba imara mpaka hali ya utulivu wa Kimbunga upite ili kujilinda wewe na familia yako.

 

9. USITOKE NJE KAMA KUNA DALILI YA NYUMBA YAKO KUSHINDWA KUHIMILI UPEPO MKALI.

Kama upepo umezidi kasi na kuelemea nyumba yako au kuhisi kuwa nyumba inataka kuanguka tafadhali usitoke nje badala yake tafuta sehemu ngumu mfano chini ya meza au kitanda na sehemu nyingine ngumu na mjibanze hapo. Ukitoka nje ni hatari maana upepo unakuja na mabati, miti na kila ghasia hivyo ni rahisi kukuvamia na kukuletea madhara makubwa kuliko kama ungebaki ndani.

 

10. JINSI YA KUTOKA NJE KAMA MAJI YANAJAA NDANI YA NYUMBA

Endapo maji yameingina na kujaa ndani ya nyumba basi hapo hakuna namna lazima mtoke nje na kutafuta hifadhi sehemu nyingine kwa maana mnaweza kuzama na kupoteza maisha. Njia ya kutoka nje ni kwa kushikana mikono na kupita pembezoni mwa nyumba taratibu. Tafadhali msipite eneo la wazi kwani hatari ni kubwa zaidi, upepo mkali huja na miti, mabati n.k. Mnapita kwa kujibanza taratibu bila kuachiana mikono muda wote hadi mfike kwenye hifadhi au sehemu salama.

-MWISHO-

 

Ee Mola wangu, nakuomba heri ya pepo hizi na heri ya vilivyomo ndani yake na heri ya shabaha ya kupelekwa kwake; na ninakuomba Unilinde na shari ya vilivyomo ndani yake na shari ya shabaha ya kupelekwa kwake.

 

Written by;

Mbega R. Ngata

email: ngatambega41@gmail.com

 

 

Refences

https://www.worldatlas.com

https://cyclonetracyinfo.weebly.com

https://www.pnbank.com.au

https://www.redcross.org.au

https://sw.wikipedia.org/wiki/Kimbunga


Submitted: April 24, 2021

© Copyright 2021 Mbega R Ngata. All rights reserved.

  • Facebook
  • Twitter
  • Reddit
  • Pinterest
  • Invite

Add Your Comments:


Facebook Comments

More Non-Fiction Articles

Other Content by Mbega R Ngata

Short Story / Romance

Short Story / Horror

Short Story / Non-Fiction