CARELESS PARENT'S

Reads: 1416  | Likes: 8  | Shelves: 0  | Comments: 0

 • Facebook
 • Twitter
 • Reddit
 • Pinterest
 • Invite

Status: Finished  |  Genre: Fan Fiction  |  House: Booksie Classic


WAZAZI WAZEMBE

CARELESS PARENT’S

Wiki kadhaa zilizopita msichana mmoja mwenye umri wa miaka 13 aligundulika kuwa ni mjamzito, wazazi wake walimuhoji lakini alikana kwa kukataa kabisa ya kwamba hajui kitu chochote kuhusu ujauzito huo. 

Walimpeleka polisi huwenda angeopa na kumtaja muhusika lakini  alipohojiwa alisema hafahamu chochote na wala hajui nini kimetokea kwake na hamfahamu mtu yoyote aliyempa huo ujauzito ni kitu amcho yeye anasema amestukia tu kuwa mjamzito.

Leo ngoja nikwambie, unafikiri ni kweli asemalo huyo binti? Hapana ukweli ni kwamba, binti uyo alipewa ujauzito na mtu wa karibu yake kabisa kwa kumlazimisha na kumtishia kuwa akisema angeweza kumdhuru na kumuahidi ahadi za uongo endapo hatamtaja.

Unafikiri nini kilitokea baada ya binti uyo kukana kumtaja muhusika? Wazazi na polisi waliamua kwenda hadi hospitali ili kuweza kupima na kuthibitisha kama hiyo mimba iliingiaje ingiaje mpaka binti huyo asijue ukweli wake.

Baada ya kumpima daktari aligundua kuwa binti hakuwa bikira na daktari amethibitisha kuwa  kuna mtu huwa anamuingilia mara kwa mara tena kwa kutumia nguvu.

Kama hiyo aitoshi, wiki mbili zilizopita msichana mwingine mdogo aliweza kufanyiwa unyama huo na mjomba wake nyumbani.

Hali kadhalika, hata mashuleni watoto wa kike hufanyiwa na baadhi ya walimu wasiokua na nia njema na kutokua waaminifu kwa watoto wa wenzao,

Mbaya Zaidi, hata majumbani kwetu kuna watu wasiokua na tabia njema kama vile baadhi ya kaka na jamaa wa karibu huwalazimisha na kuwatendea unyama huo mabinti wadogo.

Pasi kusahau vituo vya basi/daladala n.k, baadhi mambo hayo hufanyika sana na kuwaweka wasichana wengi kwenye dimbwi la mawazo na ukiwa.

Wauza magenge, mishikaki, chipsi na wengineo, baadhi yao hawapo nyuma na kushiriki haswa katika ili kwa kuwarubuni watoto.

Nilichogundua tunaishi kwenye jamii ovu na isiyokua na huruma na hofu ya Mungu, tunaishi kwenye jamii inayojijali na kutothamini umuhimu wa mwenzie hasa watoto wadogo, jamii ambayo haipishani ni muhemko ya wanyama, jamii ambayo hukandamiza na kubomoa kwa mabavu, jamii ambayo hutumia cheo / nguvu /mamlaka  kunyanya wasio kua na nguvu.

 

Ukweli ni kwamba wasichana wadogo hawapo salama kwenye kila Nyanja. Muda mwingi wapo kwenye usumbufu mkubwa sana na watu wasiokua na nia njema.

 

Je, wazazi tufanye nini???

Je, mwanao kipindi cha likizo huwa anasafiri kwenda wapi??

 • Kwa rafiki yako?
 • Shangazi yako?
 • Kaka yako?
 • Dada yako?
 • Mjomba yako?
 • Jirani yako?
 • Mchungaji?
 • Ustazi/ mwalimu wa dini?

 

Na je hao wote unawaamini watakua makini na mwanao?

Sikatai mtoto kwenda kwa ndugu zake hususani kupumzika baada ya pilika nyingi za masomo lakini je unakumbuka maneno yangu?

Tunaishi kwenye jamii ovu na isiyokua na huruma na hofu ya Mungu, tunaishi kwenye jamii inayojijali na kutothamni umuhimu wa mwenzie hasa watoto wadogo, jamii ambayo haipishani ni muhemko ya wanyama, jamii ambayo hukandamiza na kubomoa kwa mabavu , jamii ambayo hutumia cheo / nguvu /mamlaka  kunyanyasa wasio kua na nguvu.”

Ushauri wangu.

Kwa mzazi yoyote ajitahidi kuwa na mwanae angalau afike umri wa kujitambua hasa umri wa miaka 20, kutenganishwa na mtoto iwe sababu ya shule tu na sio likizo kwenda sehemu ambayo mzazi aujaifanyia utafiti wa usalama wa mwanao, kwani kuna vitu vingi sana mtoto anafanyiwa ni vigumu sana kwa mzazi kutambua na kama ukitambua unakua umeshachela.

Mfundishe mwanao wa kike kuvaa vyema na pia kuvaa akiwa ndani na sio sebleni kila mtu anamuona kwani watu wengine hawana nia njema na watoto, kuna watu wengine kazi yao ni kuwarubuni watoto

Mfundishe mwanao taadhali juu ya watu wabaya ambao wanaweza kuzoeana na mwanao kwa nia mbaya kama vile kumkumbatia na kumshika shika sehemu tofauti tofauti.

Pia kumfundsha elimu ya mahusiano na madhara yake kwa mtoto mdogo, hii itapelekea kuelewa na kuwa makini .

 

Usiwe mzazi ambaye mwenye kuficha uovu kuhofia utakua na mahusiano mabaya na jirani yako, unapaswa kukemea na kuchukua hatua kwani utawasaidia wototo wengi nyuma yako wenye tatizo kama lako

Usiwe Afisa wa polisi ambaye unaona uovu na kuutetea kwa sababu unapewa hongo, hvyo usababisha matukio kujirudia na siku yake itatokea kwenye familia yako au jamaa wa karibu yako.

Usiwe mwalimu/mfanyabiashara/kaka/baba/mjomba/babu ambaye unafanya vitendo hivyo au kufikiria kufanya hivyo ipo siku uovu utajidhihilisha.

 

Amka hakuna mtu ambaye yupo karibu na binti kama mama na baba. Usiwe mzazi mjinga kwa kumuachia mwanao hovyo. Mtoto mtunze mwenyewe kwa maadili mema na kumpatia ushauri .

Unaweza kuona kawaida lakini subiri ikukute ndio utajua ujumbe huu unamaanisha nini.

SHANGAZI, WAJOMBA, DADA, KAKA, BABA, MAMA NA WENGINE…TUUNGANE PAMOJA KUKEMEA UOVU HUU.

Imeandaliwa na Mr. Ngata kuakisi jamii ilikua ovu (Rotten society) ili kuchukua taadhali na kujifunza

Kama umeguswa unaombwa kusambaza link hii iwafikie watu wengi ili waweze kuelimika na  kwa hili.

 Pia kwa ushauri unaweza kuniandikia

Email: ngatambega41@gmail.com

Phone no. +8618627757217


Submitted: December 15, 2019

© Copyright 2021 Mbega R Ngata. All rights reserved.

 • Facebook
 • Twitter
 • Reddit
 • Pinterest
 • Invite

Add Your Comments:


Facebook Comments

More Fan Fiction Short Stories

Other Content by Mbega R Ngata

Short Story / Romance

Short Story / Horror

Short Story / Non-Fiction